Informações:
Sinopse
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episódios
-
Kwanini kampeni za mapema zimeanza nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027?
28/05/2026 Duração: 09minSiasa za kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, zimeanza kupamba moto nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya wananchi kupiga kura. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amejitokeza waziwazi na kumkosoa mrithi wake William Ruto kwa namna anavyoongoza serikali. Ruto na washirika wake, wanamtaka Uhuru kuachana na siasa. Tunachambua kauli za viongozi hao wa kisiasa.
-
Sheria mpya nchini Uganda yalenga vyama vya siasa vya upinzani
20/05/2026 Duração: 10minNchini Uganda, rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa Mei tarehe 12 kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40, ametia saini mswada tata unaolenga kudhibiti ushawishi wa kigeni nchini humo kuwa sheria. Ukiukwaji wa sheria hii mpya, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela, kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendeleza maslahi ya kigeni dhidi ya taifa la Uganda.
-
Kwanini suala la siasa na usalama, halikupewa nafasi kubwa kwenye mkutano wa Afrika na Ufaransa ?
14/05/2026 Duração: 10minMkutano wa siku mbili kati ya Ufaransa na mataifa ya Afrika, uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kati ya Mei 11 hadi 12, haukutoa kipaumbele suala la siasa na usalama katika mataifa ya Afrika, wakati huu nchi kama DRC, Sudan na yale ya ukanda wa Sahel kama Mali, Niger na Burkina Faso yakishuhudia changamoto kubwa ya kiusalama. Tunachambua kwa kina.
-
Mpango wa DRC kuwakubali wahamiaji waliofukuzwa Marekani kwazua mjadala
06/05/2026 Duração: 09minHatua ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuingia kwenye makubaliano na Marekani ili kuwapokea wahamiaji haramu waliofukuzwa nchini humo, kumezua mjadala mzito katika nchi hiyo inayoendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, hasa maeneo ya Mashariki. Kwanini kuna mvutano ?
-
Tanzania: Ripoti ya Tume imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa Oktoba 29 ?
29/04/2026 Duração: 10minNchini Tanzania Aprili tarehe 23, tume iliyoundwa kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka 2025, ilitoa ripoti yake. Kwa mujibu wa tume hiyo, watu zaidi ya 500 walipoteza maisha, maelfu walijeruhiwa huku uharibifu wa mali wenye zaidi ya thamani ya Shilingi za nchi hiyo Bilioni 125. Je, ripoti hii imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa kilichotokea nchini Tanzania ? Tunachambua.
-
Kwanini Ruben Kigame, anataka kuwa rais wa Kenya 2027 ?
22/04/2026 Duração: 10minUchaguzi Mkuu nchini Kenya ni mwezi Agosti mwaka 2027, lakini wanasiasa mbalimbali wameanza kuonesha nia ya kugombea kiti cha urais. Miongoni mwao ni Ruben Kigame, mwanasiasa, mwanaharakati, mhadhiri, mwandishi wa Habari na mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili. Yeye ni mlemavu wa Macho, ameamua kujitosa uwanjani, kutafuta uongozi wa nchi ya Kenya. Nini kimemsukuma ? Wiki hii anazungumza na mwenzangu, Benson Wakoli.
-
Mazungumzo mapya kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya DRC nchini Uswizi
15/04/2026 Duração: 10minAwamu ya tisa ya mazungumzo ya amani kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalianza siku ya Jumatatu Aprili 13 nchini Uswizi. Ujumbe wa Qatar ambao ni wasuluhishi, akiwemo mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika Massad Boulos, wanashiriki. Nini Ajenda ya mazungumzo haya ? Raia wa DRC wategeme nini ? Tunachambua.
-
Harakati za watetezi wa haki za binadamu Mashariki mwa DRC
08/04/2026 Duração: 09minMashirika ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, katika ripoti zao, yamekuwa yakionya kuwa maisha ya wanaharakati wa haki za binadamu, wana habari na viongozi wa mashirika ya kiraia yapo hatarini katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23, Mashariki mwa DRC. Wiki hii Ruben Lukumbuka, anazungumza na Jack Sinzaera, mwanaharakati maarufu kutoka Kivu Kaskazini.
-
Viongozi wa ODM wanaweza kuungana tena baada ya mpasuko wa chama ?
01/04/2026 Duração: 10minChama siasa cha Orange Democratic Movement-ODM kinaendelea kugawanyika, kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2027 nchini Kenya. Tangu kufariki dunia kwa Raila Odinga, mwasisi wa chama hicho kikubwa cha upinzani, viongozi waandamizi wa ODM wameshindwa kuelewana kuhusu kuendelea kumuunga mkono rais William Ruto, anayetarajiwa kuwania tena urais kwa muhula wa pili. Nini hatima ya chama hiki ?
-
DR Congo: Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ?
25/03/2026 Duração: 10minMjadala wa kuibadilisha katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umepamba moto. Wanasiasa wanaoegemea upande wa rais Felix Tshisekedi na chama chake cha UDPS wanaunga mkono mchakato wa katiba kubadilishwa. Upinzani wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Seneti aliyejiuzulu Modeste Bahati Lukwebo, unapinga. Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ?
-
Nini hatima ya vita vya Marekani na Israeli nchini Iran ?
18/03/2026 Duração: 10minNi wiki ya tatu sasa, baada ya Marekani na Israeli zilipoanza kutekeleza mashambulizi ya kijeshi nchini Iran. Mataifa hayo mawili yanasema lengo la mashambulizi hayo ni kuhakikisha kuwa inaharibu kabisa miundo mbinu ya Iran kutengeneza silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump, anasema vita hivi vitamalizika hivi karibuni, lakini haifahamiki ni lini. Tunachambua.
-
Kenya: Je, ushirikiano wa serikali kati ya vyama vya ODM na UDA unafanikiwa ?
11/03/2026 Duração: 10minUmepita mwaka mmoja tangu chama tawala nchini Kenya UDA na kile cha upinzani ODM, vilipoingia kwenye makubaliano ya kisiasa na kutaja mambo 10 kama vita dhidi ya ufisadi, kupunguza deni la taifa, ujumuishwaji ulio sawa serikalini kama baadhi ya mambo ya kushughulikia baada ya maandamano ya vijana ya mwaka 2024. Je, mwaka mmoja baadaye mambo hayo yametekelezwa kwa kiasi gani ? Tunachambua.
-
Nini hatima ya vita vya Israel na Marekani nchini Iran ?
04/03/2026 Duração: 10minDunia inashuhudia vita katika ukanda wa Mashariki ya Kati, baada ya Marekani na Israeli kuishambulia Iran, tangu Februari 28. Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wanataka Iran iache kutengeneza silaha za maangamizi, kuyaunga mkono makundi yenye silaha nje ya Iran na kubadilisha utawala. Kongozi wa kiroho Ayatolla Ali Khamenei, ameuawa katika vita hivyo. Nini hatima ya vita hivi ? Tunachambua.
-
Vita vya miaka minne nchini Ukraine, nini suluhu ?
25/02/2026 Duração: 09minImetia miaka minne, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, katika vita vikubwa tangu vile vya pili vya dunia barani Ulaya. Maelfu ya watu wameuawa, miji na miundo mbinu muhimu imeharibiwa nchini Ukraine. Rais Volodymyr Zelenskyy anasema mwenzake wa Urusi hajatimiza malengo yake ya vita. Kwanini suluhu haijapatikana miaka minne baadaye ?
-
Kenya: Kwanini chama cha ODM kimegawanyika kuelekea uchaguzi mkuu 2027 ?
18/02/2026 Duração: 10minJoto la kisiasa limeendelea kupanda kwenye chama cha siasa cha ODM nchini Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Chama hicho kilichoanzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Raila Odinga, kimegawanyika kwa makundi mawili. Kundi moja linaongozwa na Oburu Oginga, kaka yake Raila, linamuunga mkono rais William Ruto. Kundi lingine, linangozwa na Edwin Sifuna, Katibu Mkuu anayempinga Ruto. Nini hatima ya chama hiki ?
-
Nini kikwazo cha utekelezwaji wa mkataba wa kusitisha vita nchini DRC ?
11/02/2026 Duração: 10minWawezeshaji na wasuluhishi wa mzozo wa Mashariki mwa DRC kutoka Umoja wa Afrika, wanataka usitishwaji wa vita na utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Washington na kuheshimu mchakato wa Doha. Ni kwanini inakuwa vigumu kutekeleza mkataba huo kuheshimu maelewano ya Doha ? Tunachambua.
-
Mazungumzo ndio suluhu ya changamoto zinazoikabili DRC ?
04/02/2026 Duração: 10minRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema serikali yake ipo tayari kuongoza mazungumzo kati ya Wakongomani, ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo, hasa utovu wa usalama, mashariki mwa nchi hiyo. Hata hivyo, Chama cha "Ensemble pour la République, kinachoongozwa na mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Moise Katumbi, kinasema mazungumzo hayo yanaweza kufanyika tu iwapo yatawashirikisha wadau wote. Rais Tshisekedi, wanaotekeleza mauaji ya raia, hawapaswi kushirikishwa kwenye mazungumzo hayo. Tunachambua.
-
Kenya: Nini suluhu ya mzozo wa chama cha ODM ?
28/01/2026 Duração: 10minChama cha ODM kilichoanzishwa na aliyekuwa Waziri Mkuu nchini Kenya Hayati Raila Odinga, kinapitia mgawanyiko wa kisiasa kuhusu kumuunga mkono rais William Ruto kuwania urais kwa muhula wa pili. Viongozi wa chama hicho wamegawanyika kuhusu mpango huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Mvutano huu unamaanisha nini ?
-
Uganda: Museveni achaguliwa tena baada ya miaka 40 madarakani
21/01/2026 Duração: 10minRais Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 81, na ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 40, alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Januari 15 baada ya kupata asilimia 71.65 ya kura. Mpinzani wake wa karibu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine mwenye umri wa miaka 43, alimaliza wa pili kwa kupata asilimia 24.72 ya kura. Bobi Wine amedai kuibiwa kura. Ushindi wa rais Museveni unamaanisha nini ?
-
Uganda: Je, uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki ?
14/01/2026 Duração: 09minUchaguzi wa wabunge na urais nchini Uganda unafanyika Januari 15, 2026. Rais wa muda mrefu Yoweri Museveni ambaye ameongoza kwa miaka 40, anapambana tena na mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine. Upinzani umelalamikia kunyanyaswa, wakati huu mtandao wa Interneti ukizimwa. Je, uchaguzi huu utakuwa huru na haki ? Tunachambua kutoka Kampala.