Wimbi La Siasa

Sheria mpya nchini Uganda yalenga vyama vya siasa vya upinzani

Informações:

Sinopse

Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa Mei tarehe 12 kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40, ametia saini mswada tata unaolenga kudhibiti ushawishi wa kigeni nchini humo kuwa sheria. Ukiukwaji wa sheria hii mpya, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela, kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendeleza maslahi ya kigeni dhidi ya taifa la Uganda.