Wimbi La Siasa

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 4:02:34
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Episódios

  • Kutekwa na kufunguliwa mashtaka kwa Maduro nchini Marekani kunamaanisha nini ?

    07/01/2026 Duração: 10min

    Rais Donald Trump, Januari 3, 2026, aliagiza operesheni  maalum ya wanajeshi wa  Marekani nchini Venezuela, kumteka kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro. Baada ya kitendo hicho ambacho kimelaaniwa duniani, Maduro alisafirishwa  jijini New York na kufunguliwa mashtaka ya kuongoza biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Marekani. Tunachambua hatua hii ya rais Trump, inamaanisha nini ?

  • Matukio makubwa ya kisiasa yaliyotikisa Afrika Mashariki na Kati mwaka 2025

    31/12/2025 Duração: 10min

    Matukio makubwa ya kisiasa tuliyochambua mwaka 2025 ni pamoja na kifo cha aliyekuwa mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya Raila Odinga, uchaguzi wenye vurugu uliofanyika nchini Tanzania Oktoba 29 na kutiwa saini kwa mkataba wa kumaliza vita Mashariki mwa DRC, Desemba 04, jijini Washington DC nchini Marekani.

  • DRC: Kuondoka kwa waasi wa M23/AFC mjini Uvira kunamaanisha nini ?

    24/12/2025 Duração: 09min

    Baada ya shinikizo kutoka kwa Marekani, waasi wa M23/AFC waliondoka kwenye mji wa Uvira, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hata hivyo, rais Felix Tshisekedi ameelezea kitendo hicho kama kiini macho kwa jumuiya ya Kimataifa, kauli ambayo imeungwa na mkono na jeshi la FARDC wanaosema, waasi hao wamejificha katika milima inayopatikana na mji huo. Kuchambua kinachoendelea, tunaungana  Mali Ali akiwa  jijini Paris na François Alwende akiwa jijini Nairobi.

  • DRC: Nini hatima ya Uvira baada ya M23/AFC kuuteka mji huo ?

    17/12/2025 Duração: 10min

    Hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, si shwari licha ya kutiwa saini kwa mkataba unaolenga kusitisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miaka 30. Waasi wa M23/AFC wameudhibiti mji wa Uvira. Marekani inaonya kuichukulia hatua Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao ambao sasa wameahidi kuondoa vikosi vyake katika mji huo, lakini kwa masharti. Tunachambua kwa kina.

página 2 de 2