Habari Rfi-ki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 3:49:48
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episódios

  • Wataalamu wa afya kutoka jumuia ya EAC wakutana Mombasa pwani ya Kenya

    15/01/2025 Duração: 10min

    Makala ya habari rafiki imewashirikisha wasikilizaji kutoka kila kona ambapo wasikilizaji wametoa maoni yao kuhusu namna ambavyo wataalamu wa afya kutoka nchi za jumuia ya Afrika Mashariki walivyojadiliana kuhusu utaratibu wa kupata vibali kwenye nchi hizo bila ya kusumbuliwa. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi.

  • Kila siku ya Ijumaa kwenye makala Habari Rafiki ni Mada Huru

    03/01/2025 Duração: 10min

    Kila siku ya Ijumaa ni Mada huru  ambapo tunakupa nafasi msikilizaji kuchangia suala lolote ambalo limetokea nchini mwake au kile ambacho amekisikia katika matangazo yetu ya wiki hii.

  • Viongozi wa Afrika mashariki watoa wito wa amani kwenye hotuba ya mwaka mpya

    02/01/2025 Duração: 10min

    Katika salamu zao za mwaka mpya, viongozi karibu wote wa ukanda wa Afrika Mashariki, wametoa wito wa umoja na amani, huku kwa mataifa yenye utovu wa usalama, viongozi wakiahidi kirejesha utulivu.Tulimuuliza mskilizaji iwapo kiongozi wa nchi yake atabadili mambo mwaka huu wa 2025

  • Dunia yaukaribisha mwaka mpya wa 2025 huku viongozi wakiomba amani

    01/01/2025 Duração: 10min

    Mataifa mbalimbali duniani wakiwemo raia wa ukanda wa Afrika Mashariki, wamesherehekea mwaka mpya wa 2025 kwa kila aina ya mbwembwe na shamrashamra, kukiwa na hisia mseto za matumaini tofauti na mwaka uliopita.Tulimuuliza mskilizaji atueleze aliukaribisha mwaka mpya vipi na akiwa wapi,vile vile angependa kuona kipi kinabadilika kwenye nchi yake.

  • Matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Kenya yaibua hisia mbalimbali

    31/12/2024 Duração: 10min

    Nchini Kenya mjadala mkali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii unaendelea, ambapo baadhi wamekuwa wakiitumia kuikosoa Serikali na rais William Ruto, kwa kiwango ambacho wengine wanasema wakosoaji wamevuka mipaka huku baadhi wakisema watu wako huru kukosoa wanavyotaka.Tulimuuliwa mskilizaji je anaamini iwapo vijana wamevuka mipaka au la.

  • Umoja wa mataifa,waidhinisha kikosi kipya cha kulinda amani nchini Somalia

    30/12/2024 Duração: 10min

    Baraza la usalama la umoja wa Mataifa, mwishoni mwa juma limepitisha azimio kuunga mkono uundwaji wa kikosi kipya cha bara Afrika cha kulinda amani nchini Somalia, kikosi hiki kikichukua nafasi ya kile cha ATMIS na kitakuwa na jukumu la kuwakabili wanamgambo wa Al-Shabaab.Tumemuliza msikilizaji iwapo anaamini kikosi hiki kipya kitafanikiwa kuleta amani nchini Somalia

  • MADA HURU

    27/12/2024 Duração: 10min

    Tunakupa nafasi ya kuzungumzia tukio lolote lililotokea duniani wiki hii.  Tunakutakia sikukuu njema na maandalizi mema ya kuupokea mwaka wa 2025

  • Morocco yapendekeza wanawake kurithi mali na muda wa kuolewa kuongezwa

    26/12/2024 Duração: 10min

     Serikali ya Morocco imependekeza marekebisho ya sheria kuwaruhusu wanawake kurithi mali, umri wa kuolewa kuongezwa kutoka 17 hadi 18 na kuwekwa kwa masharti kwa wanaume wanaotaka kuoa mwanamke zaidi ya mmoja.Tunamuuliza msikilizaji maoni yake kuhusu mapendekezo hayo na hali iko vipi nchini mwake kuhusu wanawake  urithi  mali 

  • Krisimasi: Mamia ya wasafiri Kenya wakwama barabarani wakielekea sikukuu

    24/12/2024 Duração: 09min

    Mamia ya wasafiri wanaoelekea maeneo mbalimbali kwa sherehe za Krismasi wamekwama barabarani nchini Kenya kutokana na msongamano mkubwa wa magari na wengine kukosa magari ya usafiri wa umma.Tunamuuliza msikilizaji nini kinasababisha kuongezeka kwa safari msimu wa sikukuu na nchini mwao hali ikoje.

  • Habari Rafiki: Somalia kuongoza Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki

    23/12/2024 Duração: 09min

    Kwa mara ya kwanza katika historia yake, Somalia itaongoza Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki (EASF) ambacho kimetwikwa jukumu la kuimarisha amani na usalama katika eneo hilo baada ya kuchukua uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Ulinzi wa jumuiya hiyo kutoka nchi ya Rwanda katika hafla iliyofanyika jijini Kigali hapo jana.Tunamuuliza msikilizaji maoni yake ni yepi kuhusiana na hatua hii.

  • Maoni ya mskilizaji kuhusu taarifa zetu juma hili

    20/12/2024 Duração: 09min

    RFI Kiswahili kila siku ya Ijumaa inakupa nafasi ewe msikilizaji wetu kuchangia mada yeyote uliyoiskia kwenye habari zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo. Haya ndio maoni ya waskilizaji wetu juma hili.

  • Mahakama nchini Kenya yaamuru msichana wa miaka 16  anayekiri kushiriki ngono si unyanyasaji

    18/12/2024 Duração: 09min

    Wasikilizaji watoa maoni kuhusu hatua ya Mahakama moja nchini Kenya, kuamuru kwamba msichana  wa umri wa miaka 16  anayekiri kushiriki ngono na mwanaume si thibitisho la  unyanyasaji wa kigono, uamuzi ambao umeibua hisia kali nchini Kenya.

  • Rais wa Uturuki Recep Erdogan kuzuru Ethiopia na Somalia Mwakani

    18/12/2024 Duração: 10min

    Hujambo karibu katika makala ya Habari Rafiki ambapo wasikilizaji walizungumzia tangazo la Rais wa Uturuki, Recep  Tayyip Edorgan,kuwa  atazuru Ethiopia na Somalia mwakani,  baada ya kupatanisha mataifa hayo mawili kufuatia mzozo wa bandari ya Somaliland.

  • Maoni ya wasikilizaji kuhusu habari zilizogonga vichwa vya habari wiki hii

    13/12/2024 Duração: 10min

    Hapa wasikilizaji wamezungumzia mkutano kati ya viongozi wa Rwanda na DRC kule Angola wikendi hii, pia vijana kujituma ili kufanya kazi kujikimu kimaisha

  • Tanzania, Uganda na DRC zafuzu kucheza AFCON

    22/11/2024 Duração: 10min

    Hujambo na karibu kwenye makala ya habari rafiki, leo tunajadili kufuzu kwa mataifa ya Tanzania Uganda na DRCongo , kucheza kwenye mchuano ya kuwania AFCON, mataifa haya yakiwakilisha Afrika Mashariki nchini Morroco mwaka ujao.   Je unazungumziaje kufuzu kwa mataifa haya?Haya hapa baadhi ya maoni.

  • Kenya : Askofu wa kanisa katoliki walaani serikali

    19/11/2024 Duração: 09min

    Katika makala tunajadili hatua ya viongozi wa dini nchini Kenya, kutuhumu serikali kwa kile wamedai imekuwa ikitoa ahadi za uongo kwa raia. Je unazungumziaje kauli hii ya viongozi wa dini nchini Kenya? Haya hapa maoni yako.

  • Sudan : IGAD yapendekeza vikosi kutuma kulinda raia

    18/11/2024 Duração: 09min

    Kwenye makala hayai tunajadili hatua ya Jumuiya ya IGAD kuripotiwa kupendekeza kutumwa kwa wanajeshi wa kulinda amani toka nchi za Afrika ambazo hazijajihusisha kwenye mzozo unaoendelea ili kusimamia mkataba wa usitishaji mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF nchini #sudan. Unamtazamo gani kwa pendekezo hili? Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Maoni ya wasikilizaji kuhusu matukio na habari juma lote ikiwemo COP29

    15/11/2024 Duração: 10min

    Madu huru zilizoangaziwa na wasikilizaji wetu wiki hii

  • Australia imeridhia sheria kuwazuia watoto kutotumia mitandao ya kijamii

    14/11/2024 Duração: 10min

    Bunge la Australia limesema mitandao ya kijamii ina madhara makubwa kwa watoto

  • Australia yapitisha sheria ya kuwazuia watoto kutumia mitandao ya kijamii

    14/11/2024 Duração: 10min

    Bunge la Australia limesema mitandao ya kijamii ina madhara makubwa kwa watoto

página 1 de 2