Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 3:58:52
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Episódios

  • Sera za Mipango miji barani Afrika zinazingatia ustahimilivu wa majanga mijini?

    20/04/2026 Duração: 10min

    Mkutano wa pili wa Umoja wa Afrika unaofahamika kama 'Jukwaa la Mijini Afrika (AUF) ulianzishwa kwa nia ya kuwezesha mazungumzo na uratibu wa ukuaji endelevu wa miji na makazi ya watu barani Afrika. Hata hivyo miji mingi barani Afrika bado inakumbwa na majanga ya kimazingira kama vile mafuriko na uchafuzi wa hewa. Tunaangazia matokeo ya mkutano huo na ikiwa mataifa ya Afrika yana mipangilio ilio bora katika kuwezesha miji yetu kustahimili majanga ya kimazingira.

  • Ukulima wa mianzi katika kutunza mazingira ya mito nchini Kenya.

    10/04/2026 Duração: 09min

    Mimea ya mianzi yaani Bamboo ni mojawapo ya mimea kote ulimwenguni inayoweza kupandwa katika mazingira tofauti kama vile sehemu tambarare au chemichemi.   Ukulima  wa mianzi unaboresha mazingira kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo, kurejesha rotuba kwa udongo haswaa sehemu zilizo karibu na mito na hata kama kitega uchumi.

  • Manufaa ya ardhi oevu ya Ondiri kwa jamii ya kikuyu

    01/04/2026 Duração: 10min

    Katika awamu ya kwanza tuliangazia uluhimu wa maeneo ya ardhi poevu katika mazingira, ikiwa ni pamoja na kutumika kama makazi ya aina tofauti ya spishi ya viumbe hai lakini pia ni mazalia ya samaki. Sasa ardhioevu ya Ondiri ni nyumbani kwa zaidi ya spishi 90 za ndege, Kwa mfano, tulifanikiwa kumuona ndege aina ya Korongo ambao mara nyingi wao hutoroka katika ardhioevu ambayo mazingira yake yamechafuliwa. 

  • Uhifadhi wa kinamasi cha Ondiri mjini Kikuyu, nchini Kenya

    24/03/2026 Duração: 09min

    Vijana katika shirika la uhifadhi la Marafiki wa ardhi oevu ya Ondiri, ambayo ni nyumbani kwa viumbe hai na bayoanuai yenye umuhimu katika mazingira. Katika mazingira, maeneo haya yanya faida kama vile,  kufanya kazi kama sponji ya kunyonya hewa ukaa kutoka kwenye anga zaidi ya misitu ya mvua. Hutumika kama makazi ya aina tofauti ya spishi ya viumbe hai lakini pia ni mazalia ya samaki. Ardhi oevu pia hupunguza athari za mafuriko na kusafisha maji machafu.

  • Matumizi ya mitego ya wadudu inayotumia sola yaboresha parachichi na mazingira

    24/02/2026 Duração: 10min

    Wakulima wa Meru kaskazini mashariki mwa Kenya wanakumbatia matumizi ya mitego ya wadudu inayotumia nishati ya jua ili kukabiliana na false codling moth (FCM), mdudu anayeharibu mazao ya parachichi. Eneo la kaskazi mashariki huzalisha kiwango kikubwa cha parachichi zinazouzwa ulaya na Asia Kupitia teknolojia hii, wakulima  sasa wameanza kupata nafasi katika masoko ya nje....vile vile wamepunguza utegemezi wao kwa viuatilifu vya kemikali,hivyo  kuongeza kipato cha wakulima.

  • Jukumu la redio katika kuelimisha kuhusu mazingira na tabianchi

    17/02/2026 Duração: 10min

    Dunia inapokabiliwa na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi  na changamoto zingine za kimazingira, je redio imekuwa na mchango gani katika kuhakikisha jamii zinapata taarifa na habari wanazohitaji kufanya maamuzi muhimu kuhusu mazingira yao.

  • Hatau ya Marekani kujiondo kwenye mikataba ya mazingir na tabianchi na athari zake

    15/02/2026 Duração: 10min

    Aliporejea madarakani Januari 20 2025, kwa mara ya pili Trump aliiondoa Marekani katika mkataba wa tabianchi wa Paris wa 2015. Mwaka wa 2025, Washington haikuwatuma maafisa wake wa juu katika mkutano wa tabianchi wa COP30, uliofanyika Belem, Brazil. Na sasa wiki chache zilizopita, utawala wa Trump ulitangaza kuiondoa Marekani katika mashirika 66 ya kimataifa, ikiwemo ile ya UNFCCC.

  • Awamu ya pili Siku ya Kimataifa ya nishati safi 26 01 2026: Biogesi kama moja ya suluhisho

    07/02/2026 Duração: 10min

        Upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika jamii kwenye vitongoji duni. Tumetembelea mtaa wa Kawangware, jijini Nairobi, kufahamu juhudi ambazo shirika la Umande Trust linafanya katika suala zima la upatikanaji wa nishati safi kwa kuzingatia usafi wa mazingira. 

  • Siku ya Kimataifa ya nishati safi 26 01 2026: Biogesi kama moja ya suluhisho

    27/01/2026 Duração: 10min

    Upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika jamii kwenye vitongoji duni. Tumetembelea mtaa wa Kawangware, jijini Nairobi, kufahamu juhudi ambazo shirika la Umande Trust linafanya katika suala zima la upatikanaji wa nishati safi kwa kuzingatia usafi wa mazingira. 

  • Mfumo wa sola tembezi wanufaisha wakulima maeneo kame nchini Kenya

    22/01/2026 Duração: 10min

    Katika maeneo mengi ya kusini mashariki mwa Kenya, ukame na mvua zisizotabirika zimekuwa changamoto kubwa kwa wakulima. Hata hivyo, katika kijiji cha Gachuriri, Mbeere, teknolojia rahisi ya umwagiliaji  mimea maji kwa kutumia sola tembezi inayotumia nishati ya jua inaanza kubadili kilimo na kurejesha matumaini kwa wakulima wadogo.

  • Jinsi jamii ya wamasaai wanavyohamia kwenye ufugaji wa samaki baada ya mabadiliko ya tabia nchi

    18/01/2026 Duração: 09min

    Jamii ya wamaasai ambayo Kwa miaka mingi inategemea mifugo imekuwa ikipata changamoto haswa wakati wa kiangazi.  Kiangazi uathiri mifugo kwani ukosefu wa lishe unasababisha wanyama kufa. Hata hivyo Jamii hiyo imebuni mbinu mbadala ya kisasa ya ufugaji samaki. Lakini kutokana na joto jingi linaloshuhudia katika eneo la kajiado, tatizo la kuwakuza samaki hao katika vidimbwi inaonekana wazi wazi kwani wakulima hawana vifaa vya kisasa vya kupima nyuzi joto katika vidimbwi vya samaki. 

  • Awamu ya pili: Matukio muhimu ya mazingira na tabianchi mwaka wa 2025

    05/01/2026 Duração: 09min

    Katika awamu ya kwanza tuliangazia miaka kumi ya mkataba wa tabianchi wa Paris na ahadi mpya za kitaifa NDCs. Awamu  ya pili na mwisho tunaendelea kuangazia mkutano wa tabianchi COP30 uliofanyika jijini Belem, Brazil, pamoja na mkutano wa saba wa kimataifa wa mazingira UNEA-7 uliofanyika jijini Nairobi kati ya Disemba 8 na 12 ùwaka wa 2025.

  • Wanaharakati wataka uhifadhi wa msitu wa mvua wa Kongo kupewa kipaumbele

    26/12/2025 Duração: 09min

    Misitu ya mvua barani Afrika kimsingi imejikita katika Bonde kubwa la Kongo, msitu wa pili kwa ukubwa duniani wa kitropiki, unaohifadhi wanyamapori wa kipekee kama sokwe, na tembo wa msituni, pamoja na maeneo mengine muhimu kama vile Misitu ya Guinea ya Afrika Magharibi, misitu ya Afromontane Mashariki, na misitu ya pwani kutoka Kenya hadi Msumbiji yenye misitu ya kipekee ya kisiwa cha Madagaska. Mifumo hii muhimu ya ikolojia inakabiliwa na vitisho kutoka kwa ukataji miti, kilimo, na kuathiri bioanuwai yao tajiri. Kutokana na vitisho hivi wanaharakati wamepaza sauti za kulindwa kwa misitu ya mvua.

  • Lugha ya kiswahili katika kuimarisha uelewa, uhamasishaji na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

    19/12/2025 Duração: 10min

    Wakati viongozi wa dunia, wanasayansi na watunga sera wanapokutana katika miji mikuu ya Dunia kujenga hoja kuhusu hatima ya sayari kupitia mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa,  Wataalamu wa lugha,,  walimu pamoja na  wanafunzi waaendeleza  mijadala. Kaulimbiu ukiwa ni namna lugha adimu ya kiswahili inavyotumika katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

  • Kituo cha jambo Redio nchini DRC chapokea tuzo kwenye COP30

    15/12/2025 Duração: 10min

    Nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kituo cha Jambo redio, kimejitwika jukumu la kuelimisha jamii kuhusu masuala ya mazingira na tabianchi, lakini muhimu sana ni haki zao. Katika mkutano wa tabianchi uliotamatika jijini Belem nchini Brazil, kituo cha Jambo Redio kilipokea tuzo kutoka kwa shirikika linalotetea haki za wanawake Women Engage for a Common Future, WECF. Kituo hiki, kimekuwa kikitoa habari kwa jamii ambazo wakati mwingine hazina uwezo wa kupata habari.

  • COP30 uliotamatika jijini Belem, Brazil,, suala la ufadhili wa tabianchi, nishati safi ni miongoni mwa ajenda

    05/12/2025 Duração: 09min

      Miongoni mwa mambo yalioamuliwa ni kuhamasisha kiasi cha fedha trilioni 1.3 kila mwaka kufikia 2035 wa ajili ya hatua za tabianchi, kuimarisha fedha uhimilivu mara tatu kufikia 2035. Msikilizaji, suala la kuharakisha ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inasalia kuwa kipaumbele  cha dharura hasa kwa nchi zinazoendelea ambazo zina athirika pakubwa na janga hilo.

  • Shirika la Weather Mtaani labuni teknolojia ya kuepuka majanga ya hali ya hewa Kibera

    18/11/2025 Duração: 09min

    Mvua huja kwa sauti ya baraka lakini katika kitongoji, sauti hiyo hubeba hofu. Maji yanapoteremka kutoka angani, katika sekunde chache, barabara hugeuka mito. Vyumba vya kulala vinageuka mabwawa. Katika kitongoji cha Kibera jijini Nairobi nchini Kenya, hali hiyo ya hofu imebadilishwa kupitia kundi la vijana linalojiita Weather Mtaani. Shirika la Weather Mtaani linatumia teknolojia ya simu kutafsiri jumbe za utabiri wa hali ya hewa kutoka kwa mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya, kwa lugha inayoeleweka. 

  • Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP30 jijini Belem, Brazil

    12/11/2025 Duração: 09min

    Mkutano huu unakwenda kufanyika wakati ripoti mpya ya shirika la mazingira la umoja wa mataifa UNEP, ikionesha kuwa bado dunia iko nyuma katika kuafikia malengo ya mkataba wa Paris wa kudhibiti wastani wa jotoridi duniani kufikia nyuzijoto 1.5.

  • Ripoti: Matajiri wachache wanateka nyara dunia kwa kuchangia pakubwa utoaji wa hewa ukaa

    06/11/2025 Duração: 09min

    Dunia inapojiandaa kwa mkutano wa kimataifa wa Mazingira COP30 utakaofanyika Belém, Brazil, ripoti mpya imeibua mjadala mkali—si tu kuhusu uzalishaji wa hewa ukaa, bali pia kuhusu ukosefu wa usawa. Utafiti mpya wa shirika la Oxfam, unaonesha kuwa mataifa tajiri na watu wachache wenye utajiri mkubwa wanachangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabianchi. Inaitwa “ukosefu wa haki wa hali ya hewa.” Mtaalam wetu leo kulichambua hili ni David Abudho, anayeshughulika na mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika kutoka shirika la Oxfam.

página 1 de 2