Sbs Swahili - Sbs Swahili

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 108:24:34
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.

Episódios

  • Halmashauri za jiji 81 zafuta sherehe za viapo vya uraia katika siku kuu ya Australia

    26/01/2024 Duração: 08min

    Takriban halmashauri za jiji 80 kote nchini Australia, zime amua kubadili tarehe ya sherehe za kila mwaka za viapo vya uraia kutoka Januari 26.

  • Djay Daffy aweka wazi sababu za kuacha chuo

    24/01/2024 Duração: 15min

    Sekta ya burudani nchini Kenya, ina endelea kushuhudia ujio wa vijana wenye vipaji vya kila aina.

  • Taarifa ya Habari 23 Januari 2024

    23/01/2024 Duração: 24min

    Kuna taarifa serikali ya shirikisho inazingatia uwezekano wakurekebisha mpango wake wa awamu ya tatu ya makato ya kodi, muswada huo utakapo wasilishwa mbele ya baraza la mawaziri hii leo.

  • How to become a First Nations advocate - Jinsi yakuwa Mtetezi wa waAustralia wa Kwanza

    23/01/2024 Duração: 06min

    First Nations advocates help amplify the voices of Indigenous communities in Australia. Here are some aspects to consider related to advocacy and “allyship” with First Nations communities. - Watetezi wa waAustralia wa Kwanza husaidia kupaza sauti za jumuiya zawa Australia wa kwanza. Hapa kuna baadhi ya vitu vya kuzingatia kuhusiana na utetezi na “ushirika” na jumuiya zawa Australia wa Kwanza.

  • Taarifa ya Habari 19 Januari 2024

    19/01/2024 Duração: 20min

    Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema serikali ina ahidi kutimiza awamu ya tatu ya makato ya kodi, ambako wafanyakazi watapata makato ya kodi kwa mishahara yao binafsi kuanzia Julai 1.

  • Maandamano ya upizani DRC yatishia kuapishwa kwa Rais Tshisekedi

    19/01/2024 Duração: 07min

    Wawili kati ya wagombea wakuu wa upinzani kwenye uchaguzi wa Disemba mwaka jana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameitisha maandamano Jumamosi wakati wa kuapishwa kwa Rais Felix Tshisekedi kuongoza muhala wa pili.

  • Wazazi wanaweza msaidiaje mtoto kupona kiwewe?

    18/01/2024 Duração: 12min

    Iwapo mtoto wako amepata kiwewe ng'ambo au nchini Australia, iwapo ilitokea hivi karibuni au katika siku za nyuma, pakiwa msaada unao faa, mtoto anaweza pona.

  • Taarifa ya Habari 16 Januari 2024

    16/01/2024 Duração: 20min

    Wakaaji wa Magharibi Australia wame hamasishwa wapitie upya mipango yao ya moto wa vichaka, nyumba mbili zikiwa zimepotezwa kwa mioto inayo kabili eneo la kaskazini mashariki ya mji wa Perth.

  • Mwongozo wako wakubaki salama nakupata baridi wakati wa majira ya joto ya Australia

    16/01/2024 Duração: 11min

    Msimu wa majira ya joto, hu ahidi anga iliyo wazi na hali ya hewa ya joto. Kwa watu wengi, ni geuzi linalo karibishwa baada ya kuvumilia miezi ya baridi.

  • Taarifa ya Habari 12 Januari 2024

    12/01/2024 Duração: 18min

    Shirika la Human Rights Watch, limesema Australia imefeli kuchukua hatua thabiti kwa ajili yaku shughulikia swala la haki za binadam nchini China.

  • Wanafunzi wakimataifa walengwa wakuu wa mageuzi ya uhamiaji nchini Australia

    12/01/2024 Duração: 10min

    Serikali ya shirikisho imewasilisha mageuzi kadhaa kwa viza za wanafunzi wakimataifa, kama sehemu ya mageuzi makubwa ya uhamiaji yaliyo tangazwa Jumatatu 11 Disemba 2023.

  • Kila kitu una stahili jua kuhusu Boxing Day nchini Australia

    25/12/2023 Duração: 11min

    Siku ya Boxing Day nchini Australia, ni mchanganyiko wakipekee wa umuhimu wa utamaduni na biashara.

  • Krismasi huwaje nchini Australia

    23/12/2023 Duração: 08min

    Kama huwa hau sherehekei Krismasi, unaweza shangaa kuona mtu anaye vaa mavazi ya Santa akitereza juu ya maji katika mwezi wa Disemba.

  • Taarifa ya Habari 22 Disemba 2023

    22/12/2023 Duração: 16min

    Msaada wa kifedha wa ziada una tumwa kwa watu walio athiriwa kwa marufiko, wakati juhudi kubwa ya usafi ina anza katika ukanda wa Kaskazini Queensland.

  • Kanda ya Kaskazini Queensland yaanza mchakato wakufanya usafi baada ya kukumbwa kwa mafuriko

    22/12/2023 Duração: 07min

    Kiwango cha uharibifu ambao ume achwa nyuma na Kimbunga Jasper, kimeanza onekana pole pole katika kanda ya Kaskazini ya Queensland, ambako wakulima wanasema wamepoteza mazao yenye thamani ya miezi kadhaa.

  • Germain "sita ishi Kinshasa niki shinda uchaguzi, nita ishi na walio nichagua"

    19/12/2023 Duração: 16min

    Wagombea wa nyadhifa mbali mbali katika uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wame maliza kampeni zao, sasa wanasubiri hukumu ya wananchi.

  • Taarifa ya Habari 19 Disemba 2023

    19/12/2023 Duração: 18min

    Mvua kubwa na kali ambayo imegonga eneo la Kaskazini Queensland ina anza kupungua ukali ila, ofisi ya utabiri wa hewa imesema onyo za mafuriko bado zina endelea kutumika.

  • Mamba anaswa ndani ya maji ya mafuriko Kaskazini Queensland

    19/12/2023 Duração: 07min

    Mamlaka wame pata mamba wa maji ya chumvi mwenye urefu wa 2.5m, ndani ya mji wa Ingham ambao uko Kaskazini Queensland baada ya mto wa eneo hilo kufurika.

  • Taarifa ya Habari 18 Disemba 2023

    18/12/2023 Duração: 07min

    Baadhi ya wakaaji katika eneo la Kaskazini Queensland wamelazimika kupanda juu ya paa za nyumba zao, wakisubiri kuokolewa, wakati mvua nzito iliyo sababishwa na kimbunga chaki tropiki Jasper inasababisha mafuriko katika kanda hiyo.

  • Davi"tunataka badilisha muonekano kuwa lazima uwe mkonde,mwembamba na mrefu ili uwe mwanamitindo"

    15/12/2023 Duração: 16min

    Shirika la Maridadi Group, lime andaa tamasha maalum ambako wana mitindo wakike na wakiume watawania taji la Bi na Bw Kenya, Australia, 2023 mjini Melbourne, Victoria.

página 14 de 26