Sbs Swahili - Sbs Swahili
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 159:49:36
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.
Episódios
-
Australia Yafafanuliwa: Mbinu zakupunguza gharama ya mafuta
01/05/2026 Duração: 09minKuongezeka kwa bei za mafuta kunaweka shinikizo kwenye bajeti za familia kote nchini Australia—na kwa watu wengi, kunabadilisha jinsi wanavyosafiri.
-
Taarifa ya Habari: Upinzani waikosoa Serikali ya Madola kwa kuto fanya yakutosha kuimarisha usalama wa taifa
01/05/2026 Duração: 13minMbunge wa Upinzani Jonathon Duniam amesema Serikali ya shirikisho lazima iende mbali zaidi ili kuimarisha usalama wa taifa, kufuatia kutolewa kwa ripoti ya muda iliyotolewa na Tume ya Kifalme inayochunguza maswala ya chuki dhidi ya wayahudi na Uwiano wa Kijamii.
-
Yaliyojiri Afrika:Vikosi vya ulinzi vya Uganda vya shtumiwa kwa kuwauwa raia na kuwatesa wafuasi wa upinzani
01/05/2026 Duração: 07minShirika lakutetea hazi za binadam la Amnesty International, limevishtumu vikosi vya usalama vya Uganda kwa kuwauwa raia, kuwakamata kiholela na kuwatesa wafuasi wa upinzani katika kipindi chaku elekea na baada ya uchaguzi mkuu nchini humo.
-
Makala leo: Ripoti mpya yataka mkakati wa kitaifa kuhusu Akili Bandia mahali pa kazi
01/05/2026 Duração: 10minRipoti mpya inasema kwamba Australia haina mkakati wa kitaifa wa kudhibiti kuenea kwa akili bandia mahali pa kazi.
-
Tips to reduce petrol costs | Fuel in Focus - Australia Yafafanuliwa:Mbinu za kupunguza gharama ya petroli | Mafuta Yalengwa
30/04/2026 Duração: 09minRising fuel prices are putting pressure on household budgets across Australia, and for many people, it’s changing the way they travel. So what can you do to reduce your fuel costs without giving up your daily routine? Here are some simple, practical ways to save money on petrol. - Kuongezeka kwa bei za mafuta kunaweka shinikizo kwenye bajeti za familia kote nchini Australia, na kwa watu wengi, kunabadilisha jinsi wanavyosafiri. Kwa hivyo unaweza fanya nini kupunguza gharama zako za mafuta bila kuacha utaratibu wako wa kila siku? Hapa kuna njia rahisi na za vitendo za kuokoa pesa kwa petroli.
-
Taarifa ya Habari:Burundi yaanza chanjo dhidi ya saratani ya kizazi
30/04/2026 Duração: 06minWaziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anahimiza China kuanza tena usafirishaji wa mafuta ya ndege yanayo letwa Australia, baada ya mkutano na mwenzake wa China.
-
Makala leo: Matendo yakuzomea yachafua huduma za alfajiri
28/04/2026 Duração: 13minWaaustralia wameadhimisha Siku ya Anzac kote nchini na katika fukwe ya Gallipoli nchini Uturuki kuwakumbuka waliohudumu katika jeshi.
-
Wiki Hii Barani Afrika: Nchi za Afrika Mashariki kujenga kiwanda chakusafisha mafuta Tanga, Tanzania
28/04/2026 Duração: 07minBaadhi ya nchi za Afrika Mashariki zime anza mazungumzo kuhusu, ujenzi wa kiwanda chakusafisha mafuta katika bandari ya Tanga, nchini Tanzania.
-
Taarifa ya Habari: Waasi wa Touareg wachukua udhibiti wa mji wa Kidal nchini Mali
28/04/2026 Duração: 14minAustralia itatumia jumla ya dola bilioni 1.2 kutengeneza mamia ya magari ya kijeshi aina ya Bushmaster, na kuboresha magari yanayo lindwa aina ya Hawkei. Dola milioni 750 zimetengwa kutengeneza karibu magari 300 aina ya Bushmaster, ikiwa ni pamoja na magari yaliyo agizwa na serikali ya Uholanzi.
-
Makala leo: Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yavunjika tena
28/04/2026 Duração: 11minMazungumzo kati ya Marekani na Iran yamevunjika baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kutangaza Jumapili kwamba anafuta safari ya mjumbe wake kwenda Pakistan.
-
Wiki Hii barani Afrika: Somaliland tayari kuipa Marekani rasilimali zake kwa ajili yakutambuliwa kama taifa
24/04/2026 Duração: 07minUongozi wa Somalilanda, uko tayari kuipa marekani haki za kuchimba madini nakuweka kambi zaki jeshi, kwa ajili yakutambuliwa kama nchi huru.
-
SBS Learn Eng Ep 108 Jinsi yakuzungumza kuhusu gharama ya maisha
24/04/2026 Duração: 09minJe, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu gharama ya maisha ukitumia Kiingereza?
-
Taarifa ya Habari: Hatimae Tume ya Jaji Chande yatoa ripoti ya vurugu za uchaguzi Mkuu Tanzania
24/04/2026 Duração: 13minWaziri Mkuu anasema wavu wa usalama wa umma utakuwa tayari kwa wakati, kuwasaidia Waaustralia watakao ondolewa kutoka Mpango wa Bima wa Kitaifa ya Ulemavu (NDIS) yenye thamani ya mabilioni ya dola.
-
Makala leo: Watetezi waunga mkono uamuzi wa kuoga bure katika huduma ya utunzaji wa wazee nyumbani
24/04/2026 Duração: 12minWiki hii umakini mkubwa umekuwa kwenye Mfumo wa Kitaifa wa Bima ya Watu Wenye Ulemavu (NDIS), serikali ya shirikisho ikitangaza makato ambayo yanakadiriwa yata ondoa makumi ya maelfu ya watu kwenye mfumo huo.
-
The overlooked story: Aboriginal and Torres Strait Islander service on ANZAC Day - Hadithi iliyopuuzwa: Huduma yawa Aboriginal na wana Visiwa wa vya Torres Strait katika siku ya ANZAC
23/04/2026 Duração: 09minEach year Australians gather on ANZAC Day to remember those who served in wars, conflicts and peacekeeping missions. But whose stories are we remembering? Are there stories we don’t always hear? In this episode we explore an important part of Australia’s history that has often been overlooked—the service of Aboriginal and Torres Strait Islander peoples. - Kila mwaka Waaustralia hujumuika katika siku ya ANZAC kuwakumbuka waliohudumu katika vita, migogoro na misheni za kulinda amani. Lakini tunakumbuka hadithi za nani? Je, kuna hadithi ambazo hatuzisikii kila wakati? Katika makala haya tunachunguza sehemu muhimu ya historia ya Australia ambayo mara nyingi imekuwa ikipuuzwa—huduma ya watu wa Asili na wakaazi wa Visiwa vya Torres Strait.
-
Taarifa ya Habari:Waathiriwa wa maandamano wakataa mapendekezo ya sasa ya kuhusu fidia nchini Kenya
23/04/2026 Duração: 05minWaziri Mkuu Anthony Albanese amepuuza matarajio ya vikwazo vikali vya mafuta, kabla ya mkutano wa kitaifa wa baraza la mawaziri leo [[Alhamisi Aprili 23]].
-
Makala leo: Waombolezaji wa Kitaalamu wa Kenya walipwa kulia
21/04/2026 Duração: 08minUnawezaje hakikisha kwamba msiba uta hudhuriwa na watu wengi? Baada ya yote, jambo la mwisho unalotaka kutokea unapo aga dunia... ni kuondoka bila shamra shamra yoyote.
-
Wiki Hii barani Afrika:Papa Leo aomba mamlaka ya Angola kumaliza ubaguzi ambao ume endelea kusumbua nchi hiyo
21/04/2026 Duração: 06minKiongozi wa kanisa Katoliki Papa Leo XIV, amekemea vitendo vya rushwa na kuzitaka mamlaka za Angola kumaliza ubaguzi ambao ume endelea kusumbua nchi hiyo tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa mwenyewe 2002.
-
Taarifa ya Habari:Australia ya omba matokeo ya mazungumzo katika Mlango-Bahari wa Hormuz
21/04/2026 Duração: 13minWaziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anasema Australia ina omba matokeo ya mazungumzo katika Mlango-Bahari wa Hormuz, baada ya Marekani kushambulia na kukamata meli ya mizigo yenye bendera ya Iran.
-
Hadithi iliyopuuzwa: Huduma yawa Aboriginal na wana Visiwa wa vya Torres Strait katika siku ya ANZAC
20/04/2026 Duração: 11minSiku ya ANZAC ni moja ya siku muhimu zaidi za kitaifa nchini Australia. Kila mwaka, watu hukusanyika kuwakumbuka waliohudumu katika vita, migogoro na misheni za kulinda amani.