Informações:
Sinopse
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episódios
-
10 SEPTEMBA 2026
10/09/2026 Duração: 09minMada kwa kina ambayo leo inamulika jinsi Umoja wa Mataifa ulivyobaini umuhimu wa kujumuisha harakati za kutokomeza mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na usaidizi wa chakula kwa wagonjwa, familia zao na wahudumu wa afya. Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP David Stevenson ametanabaisha hayo wakati wa mahojiano yake na Dianne Penn wa Idhaa ya Kiingereza ya Umoja wa Mataifa, mahojiano ambayo yamechakatwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hili ya Kiswahili na kupatikana mada hii. Takwimu zinaonesha tangu kutangazwa rasmi kwa mlipuko huo tarehe 15 mwezi Mei mwaka huu maambukizi ni zaidi ya watu 6,686 huku waliofariki dunia ni 3,226.
-
09 SEPTEMBA 2026
09/09/2026 Duração: 09minKikosi cha 12 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia Congo DRC chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini DRC, MONUSCO kimefanikiwa kurejesha amani katika kijiji cha Sayo kilichopo katika mji wa Beni. jimboni Kivu KaskaziniTuungane na Private Lazaro Richard Mlyuka aliyetuandalia mada hii kwa kwa kina akieleza juhudi zilizofanyika na wanasaidiaje wananchi.
-
08 SEPTEMBA 2026
08/09/2026 Duração: 09minKatika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuleteaShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO linasema kuwa uvutaji sigara una uwezekano mkubwa wa kufanya iwe vigumu kwa mwanamke au mwanaume kupata mtotolikieleza kuwa wanawake wanaovuta sigara wana hatari kwa juu ya asilimia 40 kupata ugumba ikilinganishwa na wasiovuta sigara. Inakadiriwa kuwa takribani kaya moja kati ya kila kaya 4 huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, inaongozwa na mwanamke, ikiwa ni maradufu ya kiwango kilichokuwepo kabla ya kuanza kwa vita vya sasa mwezi Oktoba mwaka 2023 ambapo kaya moja kati ya kila kaya 9 ilikuwa ikiongozwa na mwanamke.Ujumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar uliokwenda Kenya kujifunza jinsi ya kuboresha mifumo ya hifadhi ya jamii hususan malipo ya fedha taslimu kwa kaya maskini, umelezea wanachoondoka nacho kupitia ziara hiyo iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP, Kenya.Na katika mada kwa kina leo Shirika la Umoja wa Ma
-
04 SEPTEMBA 2026
04/09/2026 Duração: 11minJP RWEE ni kifupi cha maneno ya lugha ya Kiingereza ambayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mpango wa Pamoja wa Kuharakisha Hatua kuelekea Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake wa Vijijini. Huu ni mpango wa kimataifa unaolenga kuhakikisha upatikanaji wa maisha endelevu na kulinda haki za wanawake wa vijijini katika muktadha wa maendeleo endelevu. Mpango huo unatekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo, FAO, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD, la masuala ya wanawake, UN Women na la Mpango wa Chakula Duniani, WFP katika nchi za Ethiopia, Guatemala, Kyrgyzstan, Liberia, Nepal, Niger, visiwa vya Pasifiki, Rwanda, Tanzania na Tunisia. Hivi karibuni tuliangazia Rwanda. Leo Anold Kayanda anatupeleka nchini Tanzania.
-
03 SEPTEMBA 2026
03/09/2026 Duração: 09minDunia iko katika mbio dhidi ya muda kuzuia ongezeko la joto duniani lisivuke nyuzi joto 1.5 Celsius. Lakini wanasayansi wanaonya kwamba kiwango hicho kinaweza kuvukwa katika miaka michache ijayo. Hali hiyo inajulikana kama “overshoot” kipindi ambacho joto duniani linapanda juu ya nyuzi joto 1.5, kabla ya kushuka tena. Je, kuvuka kiwango hicho kunamaanisha tumeshindwa? Au bado kuna nafasi ya kupunguza ukubwa wa janga hilo na kurejesha joto chini ya nyuzi joto 1.5? Katika mda hii kwa kina Flora Nducha anaangazia maana ya overshoot, madhara yake na hatua ambazo dunia inapaswa kuchukua sasa. Ungana naye
-
Kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5°C: sio sababu ya dunia kukata tamaa
03/09/2026 Duração: 06minDunia iko katika mbio dhidi ya muda kuzuia ongezeko la joto duniani lisivuke nyuzi joto 1.5 Celsius. Lakini wanasayansi wanaonya kwamba kiwango hicho kinaweza kuvukwa katika miaka michache ijayo. Hali hiyo inajulikana kama “overshoot” kipindi ambacho joto duniani linapanda juu ya nyuzi joto 1.5, kabla ya kushuka tena. Je, kuvuka kiwango hicho kunamaanisha tumeshindwa? Au bado kuna nafasi ya kupunguza ukubwa wa janga hilo na kurejesha joto chini ya nyuzi joto 1.5? Katika mda hii kwa kina Flora Nducha anaangazia maana ya overshoot, madhara yake na hatua ambazo dunia inapaswa kuchukua sasa.
-
02 SEPTEMBA 2026
02/09/2026 Duração: 11minRwanda imepiga hatua kubwa katika kuweka mfumo wa kisheria unaohakikisha wanawake na wanaume wana haki sawa za kurithi. Hata hivyo, katika baadhi ya jamii, imani za kitamaduni, mitazamo ya jadi kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume, pamoja na uelewa mdogo kuhusu sheria, bado vinaweza kuwazuia wanawake kutumia kikamilifu haki hizo.Mpango wa Pamoja wa Kuharakisha Maendeleo kuelekea Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake wa Vijijini, unaojulikana kama JP-RWEE, unaotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women), Mpango wa Chakula Duniani (WFP) pamoja na wadau wengine, kwa ufadhili wa Wakfu wa Gates, umechangia kubadilisha baadhi ya mitazamo hasi katika jamii. Anold Kayanda anasimulia kwa kina.
-
01 SEPTEMBA 2026
01/09/2026 Duração: 11minKatika Jarida la Habari za Umoja wa Mataofa hii leo Anold Kayanda anakuleteaIdadi ya vifo kufuatia mafuriko makubwa Nepal na Cina inaendelea kuongezeka kwa mujibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa sasa Nepal ni 987 na China 16 huku kukiwa na hofu kuhusu wanawake na wasichanaMashariki ya Kati hali Gaza na Ukingo wa Magharibi bado ni tete kuhusu huduma za afya na upatikanaji wa chakula na mahitaji mengine muhimu yamesema Mashirika la Umoja wa Mataifa la WFP na WHOBarani Afrika , Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Ukimwi UNAIDS, Shirika la Maendeleo la Kusini mwa Afrika SADC na China wameingia ubia wa kuimarisha teknolojia kwa ajili ya huduma za afyaNa katika mada kwa kina leo tuko Rwanda ambayo yaimarisha ubora wa kofia ngumu ili kuokoa maisha ya watumiaji wa pikipiki au bodaboda
-
31 AGOSTI 2026
31/08/2026 Duração: 11minAssumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini Burundi huko ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika anamulika sera za ujumuishi wa watu wenye ulemavu na mchango wake kwenye kufanikisha lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, la kuhakikisha kuna elimu jumuishi, bora na usawa kwa wote ifikapo mwaka 2030.
-
Mradi wa maji wa UNICEF waleta nuru kkwa wakaazi wa Garissa Kenya
29/08/2026 Duração: 02min -
UN: Mamia ya maiti wapatikana baada ya mafuriko Nepal
28/08/2026 Duração: 02min -
UNCCD: COP17 yakunja jamvi Mongolia nini kimeafikiwa
28/08/2026 Duração: 02min -
28 AGOSTI 2026
28/08/2026 Duração: 09minKatika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Nchini Nepal, warakati za uokoaji zikiendelea kuna hofu inayotanda juu ya uwezekano wa mafuriko mengine zaidi , mamia wamepoteza maisha , wengine kuokolewa na miundombinu kkusambaratishwa UN inafanya kila liwezekanalo kusaidia-Mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa katab awa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa, UNCCD COP17, umehitimishwa hii leo mjini Ulaanbaatar, Mongolia, baada ya wiki mbili za majadiliano kuhusu uharibifu wa ardhi, kuenea kwa jangwa na ukame-Na Katika Kaunti za Garissa na Mandera nchini Kenya ukame umewaweka wananchi katika changamoto ya kupata maji safi na salama, huku jamii zikilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji
-
JIFUNZE KISWAHILI - NENO KIROBEZO
27/08/2026 Duração: 45sNa sasa ni wasaa wa kujifunza Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno Kirobezo.Hili linahusu wale wanaopenda kupitapita maeneo ya watu kuvizia mlo.
-
27 AGOSTI 2026
27/08/2026 Duração: 09minLeo jaridani kuna Mada kwa Kina inakupeleka Uganda kumulika Siku ya Ziwa duniani hususan Ziwa Albert.Lakini pia kuna Muhtasari ukiwasilishwa na Leah Mushi akiangazia kumalizika kwa mlipuko wa Ebola, Uganda; Kauli ya Katibu Mkuu wa UM kuhusu maambukizi ya Ebola nchini DR Congo na kisha chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.Jifunze Kiswahili leo inabisha hodi nchini Burundi kwa Mwenyekiti wa CHAWARUNDI Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
-
26 AGOSTI 2026
26/08/2026 Duração: 09minLeo mada yetu kwa kina inaangazia mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa UNCCD COP17 unaofanyika huko mjini Ulaanbaatar, Mongolia kuanzia tarehe 17 mpaka 28 mwezi huu. Mwenzangu Leah Mushi wa idhaa hii amezungumza na wadau wanaohudhuria mkutano huo, wa kwanza anaanza kwa kujitambulisha.
-
25 AGOSTI 2026
25/08/2026 Duração: 09minUN na ICRC watoa wito mpya wa kanuni kuhusu silaha zinazojiendesha zenyewe.Mageuzi ya Kilimo ya Malawi: Mwanzo mpya kwa wakulima wadogo.Vijana wa Yambio Sudan Kusini wataka elimu, usalama na nafasi zaidi katika uamuzi.
-
24 AGOSTI 2026
24/08/2026 Duração: 09minSiku 100 tangu Ebola kutangazwa nchini DRC hali inazidi kuwa mbaya.Pamoja na kuchukua hatua WHO yaonya kuhusu kuongezeka kwa wagonjwa wa mpox Guinea-Bissau. Ufadhili mpya wa dola milioni 22 za marekani kwa elimu ya watoto walioathiriwa na mgogoro Sudan.
-
21 AGOSTI 2026
21/08/2026 Duração: 09minKatika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nduha anakuletea-Julien Harneis, Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Ebola amesema nchini DRC “Katika miezi mitatu iliyopita watu 2,500 wamekufa na nusu yao wamekufa katika kipindi cha siku tatu zilizopita na mlipuko unaendelea kusambaa zaidi, hivi sasa umesambaa katika eneo lenye ukubwa sawa na nchi ya Ufaransa.”-Hali ya ukosefu wa fedha ni mbaya pia nchini Somalia ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema kuwa kupunguzwa kwa ufadhili wa kibinadamu nchini Somalia kumesababisha kufungwa kwa vituo 205 vya afya na lishe, huku watoto wanaougua utapiamlo mkali wakisafiri umbali mrefu kutafuta matibabu wakati mwingine wakifika hospitalini wakiwa katika hali mahututi.-Leo ni ni siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Waathirika wa Ugaidi Duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amezungumzia kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Uponyaji kupitia Kumbukumbu,” akasi
-
20 Agosti 2026
20/08/2026 Duração: 11minTume ya UN: Uchaguzi Sudan Kusini usigeuke kuwa uwanja mwingine wa mapiganoWFP yaongeza operesheni za msaada kwa manusra wa teteko la ardhi ColombiaUmoja wa Mataifa na Sudan Kusini waimarisha maandalizi dhidi ya Ebola