Changu Chako, Chako Changu
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 7:59:13
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Episódios
-
Changu chako: Utamaduni wa watu kutoka Embu nchini Kenya
19/04/2026 Duração: 19minKaribu katika Makala yetu ya leo changu chako chako changu jumapili hii, Makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parle francophone na Muziki ambapo leo nitakuletea utamaduni wa watu kutoka huko Embu kwenye maswala ya chakula, mazazi na uvhumba. Tutamaliza na vibwagizo kadhaa vya Muziki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu Kumbuka pia kutufuatilia @billy bilali
-
Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa kuishi pamoja makabila mbalimbali April 12 2026
12/04/2026 Duração: 20minKaribu katika Makala yetu ya leo changu chako chako changu jumapili hii, Makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophone na Muziki ambapo leo nitakuletea utamaduni huu wa watu kutoka eneo moja kuishi pamoja mijini, na kwenye muziki nitakletea mwanaumizi Coco Finger kutoka nchini Uganda, Kumbuka kunifollow @billy bilali
-
Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa matumizi ya viungo kwenye chakula march 22 2026
21/03/2026 Duração: 20minNi jumapili nyingine tunakutana katika makala Changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali, utamaduni le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakupelekea visiwani Zanzibar kuangazia utamtuni wa matumizi ya viungo kwenye chakula, kwenye le parler francophone tutaangazia kuhusu sherehe za siku ya kimataifa ya nchi zinazo zungumza lugha ya Kifaransa, mimi ni Ali Bilali Bienvenue, ama Karibu. kumbuka pia kutufollow kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali
-
Changu Chako Chako Changu: Zanzibar yavunja rekodi ya utamaduni wa kufturisha
12/03/2026 Duração: 20minKaribu katika Makala yetu ya leo Changu Chako Chako Changu, makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakupeleka huko Visiwani Zanzibar kuzungumzia utamaduni wa kufturisha ambapo JMarch 7 umati wa watu ulijitokeza kuhudhuria Iftar ilioandaliwa kwa mara ya kwanza kwenye ngazi ya Kitaifa. Tutahitimisha na Muziki kutoka visiwani Zanzibar. Ali Bilali ninakukaribisha karibu, ama bienvenue. Utamaduni wa kufturisha ni zoezi la kijamii na kidini katika Uislamu ambapo waumini wenye uwezo hutoa chakula na vinywaji kwa waliofunga (wengine) wakati wa kuvunja saumu (futari) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Inalenga kuimarisha umoja, kusaidia wenye uhitaji, kueneza upendo, na kupata thawabu kwa kushirikiana na wengine. Utamaduni huu hufanyika kila mwaka visiwani Zanzibar, kwenye ngazi mbalimbali, kijamii, kitaasisi, lakini mwaka huu imeandaliwa Iftar ya Kitaifa, kwa mujibu wa ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar watu 27345 kati yao wanaume ni elfu
-
Changu Chako Chako Changu historia ya ngome ya Yesu Mombasa March 8
08/03/2026 Duração: 19minKatika makala yetu ya leo Jumapili mtangazaji wako Ali Bilali anatupeleka Mombasa Pwani ya Kenya kuskiliza historia ya Ngome Kongwe pamoja na ile ya ngome ya Yesu ama fort Jesus. Kumbuka pia kumfuatilia kwa kubonyeza @billy bilalihttps://www.facebook.com/billy.bilali.9
-
Changu Chako Chako Changu ukumbusho wa mizinga ya kale huko lamu Feb 15 2026
05/03/2026 Duração: 20minMakala haya mtangazaji Benson Wakoli alipata nafasi ya kutembelea county ya Lamu Pwani ya Kenya kuangazia kuhusu mizinga iliotumika zama za ukoloni. utapta pia kumsikiliza msanii kutoka nchini Burundi Baino. Kumbuka pia kunifuata @billy bilali
-
Changu Chako Chako Changu vijana wa Mombasa na fursa kwenye tasnia ya filamu Feb 1 2026
02/03/2026 Duração: 20minKatika safari yangu huko Mombasa, nimekutana na vijana kwenye tasnia ya Filamu na kufanya nao mazungumzo kuhusu tasnia hii namna inavyopiga hatuwa pamoja na chamgamoto zake. Kumbuka kutufualia @billy bilali
-
Changu chako chako changu siku ya mashujaa nchini DRC
02/03/2026 Duração: 20minMakala haya mtangazaji wako Ali Bilali anakukumbusha historia ya mashujaa nchini DRC
-
Changu Chako Chako Changu Historia na tamaduni za wabajuni march 1 2026
01/03/2026 Duração: 19minKaribu katika Makala haya Changu Chako Chako Changu Jumapili hii nakuletea Historia na tamaduni mbalimbali za watu wa kabila la wabajuni, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Maud Elka kutoka Ufaransa mwenye asili ya Congo. Watu wa Wabajuni ni kabila la Wabantu wanaoishi hasa katika jiji la Mombasa nchini Kenya. Wengi walihama kutoka kusini mwa Somalia hadi Kenya kutokana na vita na ukoo wa Waoromo wa Orma, ambao waliwafukuza kutoka eneo lao la mababu. Kundi la watu wa Bajuni hapo awali liliishi hasa Visiwa vya Bajuni katika Bahari ya Somalia. Wengi pia huishi Kenya kijadi, hasa Mombasa na miji mingine katika Mkoa wa Pwani wa nchi hiyo. Kumbuka pia kumfuatilia mtangazaji wako kwa kubonyeza hapa @billy bilali
-
Changu ChakO chako Changu waigizaji kutoka Mombasa wachangamkia fursa sehemu ya pili
28/02/2026 Duração: 20minWaigizaji wa filamu kutoka nchini Mombasa wachangamkia fursa kwa kuwezeshwa na kituo cha utamaduni wa Ufaransa Allaince Francaise ya Mombasa. Huyu hapa ni Lina Sande mmoja wapo tuliekutana naye katika ziara yetu huko Mombasa. Kumbuka pia kunifuata kwa kubonyeza hapa @billy bilali
-
Changu Chako Chako Changu fursa ya kujifunza lugha za kigeni Feb 22 2026
22/02/2026 Duração: 19minKaribu katika Makala haya Changu chako Chako Changu jumapili ya leo ambapo tumejikita zaidi katika swala la kujifunza lugha za kigeni kama Fursa. Nitakuletea pia mwanamuziki kutoka Mombasa Chikuzee, Mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu, nikukatibishe Karibu. Ama Bienvenue.
-
Baadhi ya watangazaji wa RFI Kiswahili watuma salamu za mwaka mpya 2026
04/01/2026 Duração: 19minKaribu katika Makala haya ya kwanza kabisa mwaka mwaka 2026, changu chako chako changu, nikutakie heri ya mwaka mpya. Kumbuka makala haya hukuletea historia ya mambo mbalimbali, utamaduni le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea pongezi za mwaka mpya kutoka kwa watangazaji wenzangu hapa RFI Kiswahili. Mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu, bienvenue, ama Karibu.
-
Salam za mwisho wa mwaka kutoka kwa waskilizaji wapenzi wa makala Changu Chako Dec 28
28/12/2025 Duração: 20minKaribu katika Makala haya ya mwisho kabisa katika mwaka 2025, ambapo kama ilivyo ada hukupa nafasi kutathmini ni mada gani iiokugusa katika kipindi cha mwaka 2025, lakini pia hutowa nafasi kwa waskilizaji ktoa salam za mwisho wa mwaka 2025
-
Kumbukumbu ya makala za mwaka 2025 sehemu ya pili desemba 21 2025
21/12/2025 Duração: 20minKaribu katika Makala yetu ya leo Jumapili Desemba 21, wakati tukielekea kutamatisha mwaka 2025, ambapo nakukumbusha baadhi ya makala tulizokuwa nazo mwaka huu, utapata kuskiliza makala kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini pia sehemu ya makala kuhusu mambo ambayo ni miiko kutoka makabila mbalimbali, na mwisho kabisa nitakuletea burudani ya Muziki kutoka kwake. Mimi ni A LI Bilali bienvenue ama Karibu
-
Kumbukumbu ya Makala za mwaka 2025 sehemu ya kwanza Desemba 14 2025
14/12/2025 Duração: 20minKatika Makala haya mtagazaji wako Ali Bilali anakukumbusha baadhi ya makala zilizoruka hewani katika mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya kwanza.
-
Utamaduni wa kulinda urithi na Uhifadhi wa utamaduni wa kiafrika Nov 16 2025
13/12/2025 Duração: 20minJumapili nyingine kabisa tunakutana katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni la parler francophone na Muziki Leo nakuletea utamaduni wa kulinda urithi na uhifadhi wa utamaduni wa kiafrika. Kwenye Muziki tutahitimisha na burudani kutoka mwa msanii Aslay katika kibao chake alichoshirikiana na Nandy Mimi ni Ali Bilali bienvenue, ama Karibu. .
-
Historia ya Mizinga ya lamu ndani ya makala Changu Chako Chako Changu Nov 23
13/12/2025 Duração: 20minJuma hili kupitia makala haya utapata kuskia historia ya mizinga ya Lamu huko pwani ya Kenya, lakini pia msanii Baino mzaliwa wa Burundi anaefanya muziki nchini Kenya.
-
Changu chako kuhusu maswala ya ubunifu kwenye sanaa Novemba 30
13/12/2025 Duração: 20minKaribu katika Makala Changu Chako Chako Changu Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea Maonyesho ya ushirikiano na Ufaransa na Kenya katika tasnia ya kitamaduni na ubunifu kupitia mpango wa Création Africa. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuzi Ibrah kutoka nchini Tanzania
-
Chimbuko la kabila la wanande mashariki mwa DRC na Uganda, historia maalum
07/12/2025 Duração: 20minMakala hii imeangazia kwa kina chimbuko la watu wa kabila la wanande, ambao kati yao wapo ambao wamejikita mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo maarufu kama wayira na pia wengine ambao wamejikita katika mji wa Kasese na maeneo mengine nchini Uganda na ambao wanafahamika kama Bakonzo, kufahamu zaidi sikiliza makala hii na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka.
-
Utamaduni wa wamasaai katika swala la Twahara na msanii Mistachampagne
19/11/2025 Duração: 20minMakala haya, mtangazaji wako ametembelea jijini Arusha Tanzania katika makumbusho ya Kimasai kuzungumzia mambo mbalimbali ya tamaduni za kimaasai hususan katika swala la Twahara.