Informações:
Sinopse
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episódios
-
CHAN 2024: Nani atashinda kati ya Morocco na Madagascar ?
30/08/2025 Duração: 20minMorocco na Madagascar zinachuana katika fainali ya mchezo wa CHAN 2024. Hii ni michuano inayowashirikisha wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani. Fainali hii inachezwa kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kasarani, Agosti 30 2025. Wanamichezo wetu Jason Sagini na Paul Nzioki, wanachambua kutoka uwanjani.
-
CHAN 2024: Wenyeji Kenya, Uganda na Tanzania watupwa nje ya mashindano
23/08/2025 Duração: 23minLeo tumekuandalia mengi ikiwemo kubanduliwa kwa Kenya na Tanzania kwenye michuano ya CHAN katika hatua ya robo fainali, michuano ya basketboli ya Afrika ya wanaume imeingia hatua ya nusu fainali, shirikisho la soka nchini Sudan Kusini limetangaza tarehe mpya ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya wanawake, Wan Bissaka ajumuishwa katika kikosi cha soka cha DRC, Mohammed Salah ashinda tuzo la mchezaji bora wa wachezaji kwa mara nyingine.
-
CHAN 2024: Kenya, DRC, Morocco zafukuzia ushindi mechi za mwisho za makundi
16/08/2025 Duração: 21minLeo tumekuandalia uchambuzi wa timu ambazo zimefuzu, gani zimeondolewa na nani wanaweza kufuzu hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Chan, michuano ya baskeboli ya wanaume ya Afrika, viongozi wa mashabiki Sudan Kusini waandaa mechi ya kirafiki kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, rais wa AS Kigali aahidi kuongeza tuzo za ligi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa shirikisho, Alcaraz afuzu robo fainali michuano ya Cincinnati Open.
-
CHAN 2024: Kenya yafukuzia ushindi dhidi ya Morocco, Tanzania ikihitaji sare tu
09/08/2025 Duração: 23minLeo tumekuandalia uchambuzi, matokeo na matukio ya raundi ya pili ya hatua ya makundi ya michuano ya CHAN pamoja na mechi za leo usiku na kesho mchana, droo ya michuano ya awali ya kufuzu hatua ya makundi mechi za klabu bingwa barani Afrika, uhamisho wa wachezaji Afrika Mashariki huku Kinshasa ikichaguliwa kuandaa mkutano mkuu wa CAF mwezi Oktoba, Thomas Partey kujiunga na Villareal licha ya kesi za ubakaji,